Posts

Showing posts from July, 2017

ARTESUNATE TIBA SAHIHI KWA MALARIA KALI

MALARIA NI NINI? Malaria ni ugonjwa unaosababishwa unaosababishwa na vimelea viitwavyo plasmodia. Ugonjwa huu husambazwa na mbu NINI DAWA YA MALARIA ISIYO KALI Malaria isiyo kali hutibiwa kwa dawa mseto maarufu kama Artemether lumefantrine (ALU) ZIPI NI DALILI ZA MALARTIA KALI? Kulegea kupita kiasi Mabadiliko ya tabia kama vile maluweluwe, kuhisi au kuona vitu visivyo kuwepo Kupumkua kwa shida Manjano Kutapika kila kitu Kushindwa kula au kunyonya Damu kushindwa kuzunguka mwilini Kutokwa damu kirahisi na mara kwa mara NINI TIBA SAHIHI YA MALARIA KALI Dawa ya sindano iitwayo Artesunate ndio dawa chaguo la kwanza katika kutibu malaria Dawa hii huweza kutolewa kwa njia ya mshipa au msuli kwa kipindi kisichopungua masaa 24 Baada ya hapo matgibabu hukamilishwa kwa kumpatia mgonjwa dozi kamili ya ALU HAISHAURIWI  kutumia artesunate kwa wajawazito wenye mimba iliyo na umri chini ya miezi mitatu DAWA YA KWININI ITUMIKE KWA WAJAWAZITO WENYE MIMBA YENYE UMRI CHINI YA WI...

MATUMIZI SAHIHI YA DAWA NI NINI?

Image
Matumizi ya dawa huwa sahihi pale ambapo dawa sahihi inatolewa kwa mgonjwa sahihi,kwa kiwango sahihi,kwa wakati sahihi, kupitia njia sahihi ili kutibu ugonjwa sahihi, kwa gharama sahihi Hayo yote yakifanyika kwa ufasaha basi matumizi ya dawa yanakuwa sahihi NINI FAIDA ZA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA? Huwezesha mgonjwa kutibiwa kwa usahihi Hupunguza uwezekano wa usugu wa vimelea vya magonjwa kutokea Hupunguza gharama za matibabu Hupunguza muda wa wagonjwa kulazwa hospital

Karibu pharmacist Mdugi blog

Image
Habari ndugu msomaji wa blog hii tunakukaribisha sana kwenye blog yako hii ya pharmacist Mdugi blog hii itakupa mafunzo jinsi ya kutunza afya yako.Haya yatafanyika kwa kukuelekeza matumizi sahihi ya dawa mbalimbali truzitumiazo Unatatizo lolote la kiafya basi umefika sehemu sahihi. Uliza swali lako kwenye comment hapo chini utajibiwa kwa kupewa maelezo mazuri ili tatizo lako liishe kabisa. Blog hii inaendeshwa na mtaalamu wa afya aliyebobea katika fani ya dawa (pharmacist) za magonjwa ya binadamu. Ukiwa na tangazo lolote unataka kutangaziwa kwenye blog hii inayotembelewa na maelfu ya watu kwa siku basi leta tangazo lako kwa email hii mdugig@gmail.com Utawekewa tangazo lako na kulipia pesa kidogo tu. Pia unaweza share na marafiki blog hii watumie link ya blog hii www.pharmacistmdugi.blogspot.com huko facebook twitter instagram na hata whatsapp au telegram ili jamii yote ije kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo afya kwenye blog yetu ya mtaalamu wa afya. Karibuni sana