ZITAMBUE DALILI NA ISHARA ZA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI
Upungufu wa damu mwilini huambatana na DALILI zifuatazo ; Kuchoka kirahisi Kushindwa kula na kunywa (hasa kwa watoto) Kizunguzungu na kupumua kwa shida hasa kwa akinamama wajawazito wanapofanya shughuli yoyote Historia ya kula udongo (Hasa kwa watoto na wakina mama wajawazito Ishara zifuatazo huambatana na na upungufu wa damu mwilini Weupe wa viganja, nyayo, chini ya kucha, konjactiva na ulimi Dalili za kushindwa kupumua ( kupepeta kwa pua ,kubonyea kwa kifua wakati wa kuvuta hewa, kupumua kwa shida au kutoa sauti ya kugugumia au miluzi wakati wa kuvuta hewa) Dalili za moyo kushindwa kufanya kazi kama vile ( Kupumua kwa shida ,mapigo ya moyo kwenda kasi, moyo kudunda hovyo, kuvimba mwili, kuvimba macho na ini kuuma na kuvimba linapotomaswa )