Posts

Featured post

ZIJUE FAIDA ZA KUTUMIA TANGAWIZI

Tangawizi ni moja viungo vyenye faida kubwa katika miili yetu.Tangawizi ina virutubisho muhimu kwa ajili ya mwili na ubongo wa binadamu   ZIFUATAZO NI FAIDA ZA TANGAWIZI KI AFYA Tangawizi huweza kutibu aina mbalimbali za kichefuchefu ikiwa ni pamoja na kile kisababishwacho na ujauzito (Morning sickness ) Tangawizi huweza kuondoa maumivu ya misuli ikiwa ni pamoja na yale yasababishwayo na mazoezi Inaweza kuzuia madhara yatokanayo na mfumo wetu wa kujilinda ( Anti- infammatory effects) kama vile Osteo arthritis Tangawizi inaweza kushusha kiwango cha sukari iliyozidi mwilini  Tangawizi huweza kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo Tangawizi hutibu mfumo wa mmeng'enyo wa chakula unaposhindwa kufanya kazi vizuri Tangawizi hupunguza kwa kiasi kikubwa maumivu yasababishwayo na hedhi (Dysmenorrhea) Tangawizi hupunguza uwezekano wa kupata cancer Tangawizi huimarisha uwezo wa ubongo kufanya kazi Tangawizi hupunguza cholesterol mwilini Tangawizi pia huimarisha mfumo...

ZITAMBUE DALILI NA ISHARA ZA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI

Upungufu wa damu mwilini huambatana na DALILI zifuatazo ; Kuchoka kirahisi Kushindwa kula na kunywa (hasa kwa watoto) Kizunguzungu na kupumua kwa shida hasa kwa akinamama wajawazito wanapofanya shughuli yoyote Historia ya kula udongo (Hasa kwa watoto na wakina mama wajawazito Ishara zifuatazo huambatana na na upungufu wa damu mwilini Weupe wa viganja, nyayo, chini ya kucha, konjactiva na ulimi Dalili za kushindwa kupumua ( kupepeta kwa pua ,kubonyea kwa kifua wakati wa kuvuta hewa, kupumua kwa shida au kutoa sauti ya kugugumia au miluzi wakati wa kuvuta hewa) Dalili za moyo kushindwa kufanya kazi kama vile (  Kupumua kwa shida ,mapigo ya moyo kwenda kasi, moyo kudunda hovyo, kuvimba mwili, kuvimba macho na ini kuuma na kuvimba linapotomaswa )

KWA NINI KILA MJAMZITO NI LAZIMA APEWE SP?

Image
SP (SULFADOXINE PYREMETHAMINE ) ni dawa imayotumika kama tiba ya tahadhari kwa vipindi kwa wajawazito. Kwa sasa hakuna dawa ya kinga ya ugonjwa wa malaria (Chemoprophylaxis) kwa wajawazito yenye ufanisi na usalama wa uhakika. Kwa sasa mbinu bora itumikayo ni kuondoa maambukizo ya vimelea vya malaria kwenye kondo la nyuma Maambukizi ya malaria kwenye kondo la nyuma husababisha madhara ya malaria kwenye kipindi cha ujauzito. NINI MADHARA YA MAAMBUKIZI YA MALARIA KWENYE KONDO LA NYUMA? Madhara ya maambukizi ya malaria kwenye kondo la nyuma hutokea kwa mama na kijusi nayo ni Upungufu wa damu kwa mjamzito Mtoto kuzaliwa akiwa na uzito pungufu Kijusi kufa tumboni Kuzaa kabla ya wakati Kijusi kudumaa tumboni Watoto wachanga kuzaliwa wakiwa na malaria Kwa ajili ya kuzuia madhara yatokanayo na malaria katika kipindi chote cha ujauzito, kwa uchache dozi tatu za SP zitatolewa SP HUTOLEWAJE KWA WAJAWAZITO? Kama tiba ya tahadhari kwa vipindi SP hutolewa kwa wajawazito wote kila...

PAMS foundation co-founder shot dead in Dar-es-salaam

Dar es Salaam, Tanzania We are heartbroken to share the news that PAMS Foundation co-founder, Wayne Lotter was shot and killed last night in the Masaki District of Dar es Salaam, Tanzania. Wayne devoted his life to Africa’s wildlife, from working as a ranger in his native South Africa as a young man to leading the charge against poaching in Tanzania. Wayne cared deeply about the people and animals that populate this world. In 2009, he teamed up with Krissie Clark and Ally Namangaya to form the PAMS Foundation. Together they worked tirelessly with communities in Tanzania to protect the country’s wildlife. Wayne believed communities were the best protectors of the continent’s animals. Through his work with PAMS he helped train thousands of village game scouts in every corner of the country. His ground-breaking work in developing an intelligence-based approach to anti-poaching helped successfully reverse the rampant rates of poaching facing Tanzania. Wayne’s cha...

UTI (URINARY TRACT INFECTION) NI NINI ?

Image
UTI ni maambukizi kwenye njia ya mkojo kitaalam tunaita Urinary Tract Infection. Kama wewe ni mwanamke uwezekano wa kupata maambukizi haya ni mkubwa kwa sababu za kimaumbile. SABABU ZA UTI KWA WANAWAKE Kwa wanawake njia ya mkojo (urethra) ipo karibu na njia ya haja kubwa hivyo wadudu aina ya bacteria kama E.coli wanaweza kusafiri kirahisi kutoka njia ya haja kubwa na kuingia njia ya mkojo na kusababisha maambukizi maana kwa kawaida wadudu hawa husafiri mpaka kwenye kibofu. na ndio maana baada ya kutumia maliwato wananwake hushauriwa kujifuta kutoka mbele kuelekea nyuuma kupunguza uwezekano wa maambukizi haya NINI DALILI ZA UTI ? Maumivu wakati wa kukojoa Hali ya kutaka kukojoa mara kwa mara japo mkojo hutoka kidogo Maumivu ya mgongo na sehemu ya chini ya tumbo Mkojo mchafu na wenye harufu isiyo ya kawaida Kujisikia mchovu na homa UCHUNGUZI Unapohisi dalili hizi wahi hospitali ambako utaombwa utoe mkojo utakao fanyiwa uchunguzi ili kubaini uwepo wa wadudu wanaosababis...

ARTESUNATE TIBA SAHIHI KWA MALARIA KALI

MALARIA NI NINI? Malaria ni ugonjwa unaosababishwa unaosababishwa na vimelea viitwavyo plasmodia. Ugonjwa huu husambazwa na mbu NINI DAWA YA MALARIA ISIYO KALI Malaria isiyo kali hutibiwa kwa dawa mseto maarufu kama Artemether lumefantrine (ALU) ZIPI NI DALILI ZA MALARTIA KALI? Kulegea kupita kiasi Mabadiliko ya tabia kama vile maluweluwe, kuhisi au kuona vitu visivyo kuwepo Kupumkua kwa shida Manjano Kutapika kila kitu Kushindwa kula au kunyonya Damu kushindwa kuzunguka mwilini Kutokwa damu kirahisi na mara kwa mara NINI TIBA SAHIHI YA MALARIA KALI Dawa ya sindano iitwayo Artesunate ndio dawa chaguo la kwanza katika kutibu malaria Dawa hii huweza kutolewa kwa njia ya mshipa au msuli kwa kipindi kisichopungua masaa 24 Baada ya hapo matgibabu hukamilishwa kwa kumpatia mgonjwa dozi kamili ya ALU HAISHAURIWI  kutumia artesunate kwa wajawazito wenye mimba iliyo na umri chini ya miezi mitatu DAWA YA KWININI ITUMIKE KWA WAJAWAZITO WENYE MIMBA YENYE UMRI CHINI YA WI...

MATUMIZI SAHIHI YA DAWA NI NINI?

Image
Matumizi ya dawa huwa sahihi pale ambapo dawa sahihi inatolewa kwa mgonjwa sahihi,kwa kiwango sahihi,kwa wakati sahihi, kupitia njia sahihi ili kutibu ugonjwa sahihi, kwa gharama sahihi Hayo yote yakifanyika kwa ufasaha basi matumizi ya dawa yanakuwa sahihi NINI FAIDA ZA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA? Huwezesha mgonjwa kutibiwa kwa usahihi Hupunguza uwezekano wa usugu wa vimelea vya magonjwa kutokea Hupunguza gharama za matibabu Hupunguza muda wa wagonjwa kulazwa hospital