KWA NINI KILA MJAMZITO NI LAZIMA APEWE SP?
SP (SULFADOXINE PYREMETHAMINE) ni dawa imayotumika kama tiba ya tahadhari kwa vipindi kwa wajawazito.
Kwa sasa hakuna dawa ya kinga ya ugonjwa wa malaria (Chemoprophylaxis) kwa wajawazito yenye ufanisi na usalama wa uhakika.
Kwa sasa mbinu bora itumikayo ni kuondoa maambukizo ya vimelea vya malaria kwenye kondo la nyuma
Maambukizi ya malaria kwenye kondo la nyuma husababisha madhara ya malaria kwenye kipindi cha ujauzito.
NINI MADHARA YA MAAMBUKIZI YA MALARIA KWENYE KONDO LA NYUMA?
Madhara ya maambukizi ya malaria kwenye kondo la nyuma hutokea kwa mama na kijusi nayo ni
SP HUTOLEWAJE KWA WAJAWAZITO?
Kama tiba ya tahadhari kwa vipindi SP hutolewa kwa wajawazito wote kila wanapohudhuria kliniki ya wajawazito kama ifuatavyo
Hivyo basi ni muhimu kwa wajawazito wote kupata SP ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza kwa sababu ya maambukizi ya malaria kwenye kondo la nyuma

- Upungufu wa damu kwa mjamzito
- Mtoto kuzaliwa akiwa na uzito pungufu
- Kijusi kufa tumboni
- Kuzaa kabla ya wakati
- Kijusi kudumaa tumboni
- Watoto wachanga kuzaliwa wakiwa na malaria
SP HUTOLEWAJE KWA WAJAWAZITO?
Kama tiba ya tahadhari kwa vipindi SP hutolewa kwa wajawazito wote kila wanapohudhuria kliniki ya wajawazito kama ifuatavyo
- Angalau dozi tatu za SP hutolewa katika kipindi chote cha ujauzito
- Dozi ya kwanza ya SP hutolewa katika hudhurio la wiki ya 14 ya umri wa ujauzito
- Huwa kunakuwa na kipindi cha mwezi mmoja kati ya dozi moja ya SP na nyingine
- Dozi ya mwisho ya SP hutolewa hata kwa kuchelewa bila hofu ya usalama ( Juma la 36)
- Wanaotumia dawa ya Co-trimoxazole kama kinga huwa hawapewi SP
Hivyo basi ni muhimu kwa wajawazito wote kupata SP ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza kwa sababu ya maambukizi ya malaria kwenye kondo la nyuma

Comments
Post a Comment