ZITAMBUE DALILI NA ISHARA ZA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI
Upungufu wa damu mwilini huambatana na DALILI zifuatazo ;
- Kuchoka kirahisi
- Kushindwa kula na kunywa (hasa kwa watoto)
- Kizunguzungu na kupumua kwa shida hasa kwa akinamama wajawazito wanapofanya shughuli yoyote
- Historia ya kula udongo (Hasa kwa watoto na wakina mama wajawazito
- Weupe wa viganja, nyayo, chini ya kucha, konjactiva na ulimi
- Dalili za kushindwa kupumua ( kupepeta kwa pua ,kubonyea kwa kifua wakati wa kuvuta hewa, kupumua kwa shida au kutoa sauti ya kugugumia au miluzi wakati wa kuvuta hewa)
- Dalili za moyo kushindwa kufanya kazi kama vile ( Kupumua kwa shida ,mapigo ya moyo kwenda kasi, moyo kudunda hovyo, kuvimba mwili, kuvimba macho na ini kuuma na kuvimba linapotomaswa )
Comments
Post a Comment