UTI (URINARY TRACT INFECTION) NI NINI ?
UTI ni maambukizi kwenye njia ya mkojo kitaalam tunaita Urinary Tract Infection.
Kama wewe ni mwanamke uwezekano wa kupata maambukizi haya ni mkubwa kwa sababu za kimaumbile.

SABABU ZA UTI KWA WANAWAKE
Kwa wanawake njia ya mkojo (urethra) ipo karibu na njia ya haja kubwa hivyo wadudu aina ya bacteria kama E.coli wanaweza kusafiri kirahisi kutoka njia ya haja kubwa na kuingia njia ya mkojo na kusababisha maambukizi maana kwa kawaida wadudu hawa husafiri mpaka kwenye kibofu.
na ndio maana baada ya kutumia maliwato wananwake hushauriwa kujifuta kutoka mbele kuelekea nyuuma kupunguza uwezekano wa maambukizi haya
NINI DALILI ZA UTI ?
UCHUNGUZI
Unapohisi dalili hizi wahi hospitali ambako utaombwa utoe mkojo utakao fanyiwa uchunguzi ili kubaini uwepo wa wadudu wanaosababisha UTI.
MATIBABU
Ukibainika kuwa na maambukizi haya dawa aina ya antibiotics hutolewa ili kuua wadudu hawa.Hakikisha unatumia dawa hizi kadiri ya maelekezo ya mtoa huduma wa afya ili kutibu kwa ufasaha na kuzuia uwezekano wa usugu wa vimelea kujitokeza
Pia tabibu anaweza kutoa dawa za kutuliza maumivu ili kumpunguzia mgonjwa maumivu

- Maumivu wakati wa kukojoa
- Hali ya kutaka kukojoa mara kwa mara japo mkojo hutoka kidogo
- Maumivu ya mgongo na sehemu ya chini ya tumbo
- Mkojo mchafu na wenye harufu isiyo ya kawaida
- Kujisikia mchovu na homa
UCHUNGUZI
Unapohisi dalili hizi wahi hospitali ambako utaombwa utoe mkojo utakao fanyiwa uchunguzi ili kubaini uwepo wa wadudu wanaosababisha UTI.
MATIBABU
Ukibainika kuwa na maambukizi haya dawa aina ya antibiotics hutolewa ili kuua wadudu hawa.Hakikisha unatumia dawa hizi kadiri ya maelekezo ya mtoa huduma wa afya ili kutibu kwa ufasaha na kuzuia uwezekano wa usugu wa vimelea kujitokeza
Pia tabibu anaweza kutoa dawa za kutuliza maumivu ili kumpunguzia mgonjwa maumivu

Being clean is important to avoid such infections
ReplyDelete